Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Polisi Wamshikilia Leonard Magere wa Chadema kwa Tuhuma za Jinai

  • 31
Scroll Down To Discover

Jeshi la Polisi Tanzania limethibitisha kumshikilia Mtaalamu wa Raslimali, Miradi na Uwekezaji wa Chama Cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA), Leonard Magere kwa tuhuma za jinai zinazomkabili.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Julai 13,2025 kwa vyambo vya habari na Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, Makamo Makuu ya Polisi, Magere alikamatwa Julai 12,2025 kutokana na tuhuma za jinai zinazomkabili.

“Zipo taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikitaka kufahamu kama ni kweli Leonard amekamatwa na Jeshi la Polisi. Jeshi la Polisi Nchini ningependa kueleza kuwa ni kweli Leonard alikamatwa jana Julai 12,2025 kutokana na tuhuma za jinai zinazomkabili na anaendelea kushikiliwa kwa mahojiano ili kukamilisha ushahidi ambao ulishakusanywa,”imefafanua taarifa hiyo.

Taarifa kwa umma ya Julai 12, mwaka huu iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Diaspora, John Kitoka imeeleza kuwa Magere alizuiliwa na mamlaka ya uhamiaji kusafiri kuelekea nchini Uingereza usiku huu.

Siku hiyo hiyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia, alizuiwa katika mpaka wa Namanga, mkoani Arusha wakati akisafiri kwenda nchini Kenya.



Prev Post KISA YANGA…..NZENGELI AIPIGA CHINI OFA YA MIL 600 KUTOKA SIMBA…ISHU NZIMA IKO HIVI…
Next Post Makalla: Tumeisoma Barua ya Polepole Mtandaoni, Lakini Bado Ni Mwanachama wa CCM – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook