Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Makalla: Tumeisoma Barua ya Polepole Mtandaoni, Lakini Bado Ni Mwanachama wa CCM – Video

  • 45
Scroll Down To Discover

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM anayeshughulikia Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA. Amos Makalla, amesema kuwa taarifa ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Mhe. Humphrey Polepole, bado haijathibitishwa rasmi na mhusika, licha ya kusambaa mitandaoni.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo, Makalla amesema kuwa yeye, kama wananchi wengine, ameisoma barua hiyo kupitia mitandao ya kijamii na hawezi kuthibitisha uhalali wake hadi itakapothibitishwa na Mhe. Polepole mwenyewe.

“Nikiri kuisoma barua ya Polepole kwenye mtandao kama ulivyoisoma wewe. Mtu wa kuthibitisha uhalali wa barua hiyo ni yeye mwenyewe. Lakini sisi tumeisoma, na maudhui yake nimeyasoma. Naamini mtapata nafasi ya kujiridhisha kama barua hiyo ni ya kweli,” alisema Makalla.

Ameeleza kuwa iwapo ni kweli, basi ni wazi kwamba aliyoyasema ni maoni binafsi ya Mhe. Polepole, na Chama Cha Mapinduzi kinayaheshimu kama sehemu ya uhuru wa mwanachama kutoa mawazo.

“Kama ni ya kweli, basi yale ni mawazo yake. Lakini jambo kubwa ambalo limenifurahisha ni pale aliposema kwamba atabaki kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi. Tunamshukuru kwa hilo,” aliongeza.

CPA. Makalla alisisitiza kuwa Mhe. Polepole bado ni mmoja wa wanachama wa CCM kati ya wanachama zaidi ya milioni 13 waliopo nchini, na kwamba Chama kitaendelea na shughuli zake za kawaida ikiwemo mchakato wa kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao.

“Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Mgombea Mwenza ni Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi. Mgombea wa Zanzibar ni Dkt. Hussein Mwinyi. Mchakato unaendelea,” alieleza.

Makalla pia alisisitiza kuwa Chama kipo imara na kinaendelea na maandalizi ya uchaguzi kwa misingi ya utulivu, mshikamano na mshindano ya kistaarabu.



Prev Post Polisi Wamshikilia Leonard Magere wa Chadema kwa Tuhuma za Jinai
Next Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO JULAI 14, 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook