Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

KISA ENG HERSI…..SIMBA KULAMBA MAMILIONI KUTOKA CAF….ISHU NZIMA IKO HIVI…

  • 56
Scroll Down To Discover

Mwaka uliopita, Chama cha Umoja wa Vilabu Afrika (ACA) chini ya uongozi wa Eng. Hersi Said, kilifanikiwa kushawishi CAF kutoa dola 50,000 kwa kila klabu iliyoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL) na Kombe la Shirikisho (CAF CC) katika hatua ya awali.

Kwa msimu huu mpya, ACA imeendelea kupigania maslahi ya vilabu barani Afrika kwa mafanikio zaidi. Kupitia mazungumzo na ushawishi wao kwa CAF, imeidhinishwa kuwa klabu zitakazoshiriki hatua ya awali ya CAF CL na CAF CC zitalipwa dola 100,000 sawa na zaidi ya Milioni 270 kila moja kwa ajili ya maandalizi.

Ikumbukwe, kabla ya uwepo wa ACA, klabu shiriki katika hatua za awali za mashindano hayo hazikuwa zikipewa msaada wowote wa kifedha na CAF.

Hatua hii imepongezwa na wadau wengi wa soka barani Afrika kama ishara ya kweli ya mapambano ya kuleta usawa na maendeleo ya vilabu vya Afrika vilivyo katika mazingira magumu ya kifedha.

Kwa mara nyingine tena, Eng. Hersi Said ameendelea kuthibitisha kujitolea kwake kwa dhati katika kuendeleza soka la Afrika na kupigania maslahi ya vilabu.

“Hersi anazidi kuipambania football ya Afrika.” – @alikamwe

The post KISA ENG HERSI…..SIMBA KULAMBA MAMILIONI KUTOKA CAF….ISHU NZIMA IKO HIVI… appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post KISA UKIMYA MWINGI….SIMBA WAIBUKA NA HILI JIPYA….ISHU YA FADLU KUSEPA HII HAPA…
Next Post MERIDIANBET WAJA NA SUPER HELI, USHINDE SAMSUNG A25 BILA KUTOA JASHO…
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook