

Wakazi wa jiji la Nairobi nchini Kenya leo Julai 7 , 2025 wamekuwa wakisikiliza milio ya bunduki na mabomu ya kutoa machozi ikilipuliwa tangu asubuhi kutoka barabara kuu ambako makundi ya vijana wamekuwa waking’ang’ana kulazimisha kupita ili kulifikia eneo la katikati ya jiji.
Hali ya taharuki imetanda kote katika jiji kuu la Kenya nairobi, huku polisi wakikabiliana na waandanamanaji vijana wa Gen Z wanaotaka kuingia mjini humo kuelezea kero zao.
Maandamano haya yanafanyika katika siku ya Saba Saba, inawakilisha tarehe 7 Julai, siku inayotumika kama ukumbusho mkubwa wa kujitolea kwa Wakenya katika mapambano ya demokrasia ya vyama vingi.

Wafanyabiashara wamelazimika kufunga biashara zao yakiwemo maduka ili kuepuka wizi na uharibifu wa mali zao unaotawala kila mara maandamano yanapofanyika jijini. Kwa kiasi kikubwa polisi wameweza kudhibiti maandamano hayo kwa kuwazuia vijana wa Gen Z kuingia jijini.
Polisi wameweka vizuizi katika barabara zote zinazoingia jijini, kupiga doria kwa helikopta za kijeshi na kuzuia safari zote za kuelekea jijini Nairobi, isipokuwa usafiri wa pikipiki.

Baadhi yao wafanyabiashara wamechukua jukumu la kulinda mali zao dhidi ya wahuni wanaoambata na wandamanaji na kuiba mali zao
Awali Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Gilbert Masengeli alikanusha madai kwamba Wakenya wanazuiwa kuingia katikati ya jiji la Nairobi, akisema watu wanaendelea kwenda jijini bila vikwazo.

Huduma ya Kitaifa ya Polisi imetoa wito kwa Wakenya kudumisha amani na kujizuia wakati wa siku ya Saba Saba hii leo.
Katika taarifa ya polisi kuhusu maandimisho ya Saba Saba iliyotolewa hapo jana, polisi ilitoa hakikisho la kujitolea kwao kulinda maisha na mali ya Wakenya wote, kudumisha amani, sheria, na utaratibu.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!