
Takribani watu watatu wanahofiwa kufariki dunia kufuatia ajali mbaya iliyotokea leo, Julai 7, 2025, katika eneo la Mtoni Msikitini, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili T617 DUL, ambalo lilipoteza mwelekeo na kugonga lori lenye namba T322 AVV, pamoja na Bajaj mbili na bodaboda mbili.
Inadaiwa kuwa watu waliopoteza maisha walikuwa wakisafiri kwa bodaboda zilizogongwa kwa nyuma na gari hilo, kisha kurushwa hadi kugonga lori.
Global TV imefika eneo la tukio na kushuhudia miili ikiondolewa barabarani, huku pia magari, Bajaj, na bodaboda zilizohusika kwenye ajali hiyo zikitolewa ili kuruhusu barabara, ambayo ilikuwa imefungwa kwa muda, ifunguliwe na magari yaendelee na safari.
Hadi sasa, mamlaka husika bado hazijatoa taarifa rasmi kuhusu idadi kamili ya waliopoteza maisha au hatua zilizochukuliwa kufuatia ajali hiyo.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!