Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Polisi Wamkana Aliyedaiwa Kuwa Mkuu Wa Kituo Cha Polisi Tabora – Video

  • 32
Scroll Down To Discover

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limetoa taarifa kuhusu picha mjongeo (video clip) inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, ikiwa na kichwa cha habari: “Mkuu wa Kituo cha Polisiu Tabora Amuomba Msamaha Heche Baada ya Vurugu.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limewataka wananchi kuipuuza picha hiyo ya mjongeo, kwani imetengenezwa kwa lengo la kuwadanganya na kuwapotosha.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora halina Mkuu wa Kituo cha Polisi wa aina hiyo kama anavyoonekana kwenye video hiyo.

Kutokana na kitendo hicho cha kihalifu cha kutengeneza na kusambaza taarifa za uongo, Jeshi la Polisi limefanya msako na kufanikiwa kumkamata mtu aitwaye Daudi Paul Delim (49), mkazi wa Mbagala A, wilayani Igunga, ambaye alijifanya kuwa Mkuu wa Kituo cha Polisi na kuonekana akiomba msamaha.

Mtuhumiwa amekamatwa na anaendelea kuhojiwa ili kubaini aliowashirikiana nao kutengeneza na kusambaza picha hiyo ya mjongeo yenye maudhui hasi na ya kupotosha, ili hatua stahiki za kisheria zichukuliwe dhidi yao.



Prev Post Mazishi ya Lungu yazua kutoelewana na serikalli ya Zambia
Next Post MAGAZETI ya Leo Alhamisi 12 June 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook