Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Binti wa Rais Paul Biya Aomba Umma Wasimpigie Kura Baba Yake

  • 2
Scroll Down To Discover

Yaoundé – Dunia imetaharuki baada ya Brenda Biya, binti wa Rais wa Cameroon Paul Biya, kuwataka wananchi wa nchi hiyo wasimpigie kura baba yake katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.

Kupitia video aliyoipakia kwenye TikTok, Brenda anayejulikana mtandaoni kama “King Nasty”, alimlaumu baba yake kwa kusababisha umasikini wa wananchi, ukosefu wa ajira na kudorora kwa maendeleo nchini humo.

Tukio hili limeelezwa kuwa la kwanza barani Afrika ambapo mtoto wa rais aliye madarakani anampinga waziwazi mzazi wake kisiasa.

Rais Paul Biya, mwenye umri wa miaka 92, amekuwa madarakani tangu mwaka 1982, akitazamwa na wengi kama mmoja wa viongozi waliodumu madarakani kwa muda mrefu zaidi duniani.

Hata hivyo, wakosoaji wamesema kuwa Brenda, ambaye anaishi ughaibuni kwa maisha ya kifahari, hana uhusiano wa karibu na familia yake na huenda kauli yake isiakisi kwa usahihi hali halisi ya wananchi wa Cameroon.

Kwa sasa kauli hiyo imeibua mjadala mpana ndani na nje ya Cameroon, ikitazamwa kama changamoto ya kipekee kwa urithi wa kisiasa wa Rais Biya.

MANENO ya RC CHALAMILA MSIBANI kwa MASISTA WALIOFARIKI kwa AJALI -“KANISA la MUDA-TUNACHANGIA MIL



Prev Post TLS Yakutana Na Kufanya Mazungumzo Na Jaji Mkuu Wa Mahakama Ya Tanzania
Next Post Askofu Novatus Rugambwa Kuagwa Dar, Kuzikwa Bukoba
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook