Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Polisi Iringa: Watuhumiwa 15 wakamatwa kwa mauaji ya kijana – Video

  • 4
Scroll Down To Discover

Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa limetoa taarifa kuhusu video iliyosambaa mitandaoni ikimuonyesha kijana akipigwa na wananchi waliokuwa wakijichukulia sheria mkononi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa amesema uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa kijana huyo ni Yohana Mgaya (14), mkazi wa Don Bosco, Kata ya Mkwawa, Manispaa ya Iringa.

Marehemu alihusishwa na matukio ya wizi wa mali mbalimbali ikiwemo vifaa vya bajaji, nguo, simu na matunda aina ya parachichi.

Polisi wamesema wamefanikiwa kuwakamata jumla ya watuhumiwa 15, akiwemo Erasto Kilamlilo (46), mkazi wa Don Bosco, na wenzake 14 walioshiriki katika shambulio lililosababisha kifo cha kijana huyo Septemba 11, 2025.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi, uchunguzi wa shauri hilo bado unaendelea ikiwa ni pamoja na kukusanya vielelezo mbalimbali.

Imebainika pia kuwa marehemu alikuwa ameachiwa gerezani mwezi Julai mwaka huu baada ya kukamatwa kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.



Prev Post Eric Shigongo kuzungumzia fursa za Afrika katika jukwaa la kimataifa la ujasiriamali
Next Post Mtambo Wa Gesi Asilia Wasafirishwa Kwenda Mtwara Kuongeza Nguvu Ya Uzalishaji Wa Umeme
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook