Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Nchi za Kiarabu Zashambulia Kauli ya Upanuzi wa Mipaka ya Israel

  • 4
Scroll Down To Discover

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amezua taharuki na ukosoaji mkali kutoka kwa nchi kadhaa za Kiarabu baada ya kusema kuwa anajihusisha sana na maono ya ‘Israeli Kubwa’ (Greater Israel), kauli ambayo imechukuliwa kama ishara ya misimamo ya kupanua mipaka ya Israel hadi maeneo ya nchi jirani.

Kauli hiyo aliitoa Jumanne usiku katika mahojiano na kituo cha televisheni cha i24News, ambapo alijibu kwa ‘sana’ alipoulizwa iwapo anahisi uhusiano na wazo hilo.

‘Israeli Kubwa’ ni dhana yenye tafsiri mbalimbali, ikiwemo madai ya Israel kudai maeneo yanayozunguka nchi hiyo kwa misingi ya kihistoria au Biblia.

Baadhi ya tafsiri zake hujumuisha maeneo ya Jordan, Lebanon, Syria, Misri, Iraq na hata Saudi Arabia.

Dhana hiyo ilipata nguvu zaidi baada ya Vita ya Siku Sita mwaka 1967, ambapo Israel iliteka maeneo kama Ukanda wa Gaza, Ukingo wa Magharibi, Jerusalem Mashariki, Rasi ya Sinai na Milima ya Golan.

Kauli ya Netanyahu ilitolewa baada ya mtangazaji Sharon Gal – ambaye aliwahi kuwa mbunge wa mrengo wa kulia – kumpa zawadi ya hirizi inayodaiwa kuwa na ramani ya “Ardhi ya Ahadi,” ambayo haikuonyeshwa hadharani.

Gal anadaiwa kuuza mikufu yenye ramani hiyo yenye taswira ya Israel iliyopanuliwa.

Matamshi hayo yamekumbwa na ukosoaji mkubwa kutoka kwa nchi za Kiarabu ikiwemo Saudi Arabia, Qatar, Jordan, Misri pamoja na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League), ambazo zimezitaja kuwa za kichochezi, za hatari na kinyume na juhudi za kutafuta amani.

Jordan, kupitia msemaji wa wizara ya mambo ya nje, Sufyan Qudah, ilisema kauli hizo ni ‘hatari’ na ‘uchochezi’, ikieleza kuwa zinachochea mzunguko wa migogoro na vurugu katika eneo hilo.

Misri nayo ilitaka Israel kutoa ufafanuzi kuhusu kauli hiyo na kusema inapingana na matarajio ya amani ya nchi za eneo hilo na jumuiya ya kimataifa.

Qatar nayo ilitoa tamko kali ikieleza kuwa matamshi hayo yanaendeleza kiburi cha kiukaliaji, na hayataweza kudhoofisha haki halali za mataifa ya Kiarabu. Iliongeza kuwa inasimamia juhudi zote za kufanikisha amani ya haki na ya kudumu katika eneo hilo.

Saudi Arabia ilikemea vikali kauli hizo na kuonya kuwa mipango ya upanuzi ya Israel ni tishio kwa usalama wa kikanda na wa kimataifa.



Prev Post Putin Asifu Juhudi za Trump Kumaliza Vita vya Ukraine
Next Post Yanga Yatoa Ufafanuzi Kuhusu Mchango wa CCM wa Shilingi Milioni 100
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook