
Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino, ametoa wito wa amani duniani, akisisitiza haja ya kulinda utu wa binadamu hasa kwa watoto na kina mama wanaoteseka kutokana na vita na migogoro.
Akizungumza katika mkutano wa Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York, Infantino alisema:
“Sote tunajua kwamba tunaishi katika ulimwengu uliogawanyika, ulimwengu mkali, ulimwengu mgumu. Na kama ninyi nyote, ninateseka ninapoona watoto wakiteseka na akina mama wakilia.”
Katika mjadala huo, wataalamu wa Umoja wa Mataifa waliomba FIFA na UEFA kuchukua hatua kali dhidi ya Israel kwa kuisimamisha kushiriki mashindano ya kimataifa ya kandanda, wakisema ni jibu la lazima kutokana na kile walichokiita “mauaji ya kimbari yanayoendelea katika ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu.”
Hatua hii inakuja wakati migogoro katika Sudan, Gaza na maeneo mengine yenye mizozo duniani ikiendelea kuleta athari kubwa kwa raia wasio na hatia.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!