Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Moto Waua Watoto 5 Bwereni Kituo cha Yatima Tabora

  • 34
Scroll Down To Discover

Watoto watano wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa baada ya bweni la Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Igambilo, kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo Julai 29, 2025 Kata ya Misha, Mkoani Tabora.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 5 usiku wakati watoto wakiwa wamelala. Wananchi wa eneo hilo walianza kuzima moto kabla ya kufika kwa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji.

Chanzo cha moto bado hakijathibitishwa rasmi, lakini taarifa za awali zinaeleza kuwa huenda kimesababishwa na hitilafu ya umeme.

Majeruhi wamepelekwa hospitalini kwa matibabu, huku uchunguzi wa tukio ukiendelea.

Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV — usisahau ku-like, ku-comment na ku-subscribe ili uendelee kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.

 



Prev Post CCM Yatoa Orodha ya Wagombea Ubunge Uchaguzi Mkuu 2025, Majina Yapo Hapa Majimbo Yote – Video
Next Post MONUSCO Yalaani Mauaji ya Raia 43 Kwenye Shambulio la ADF Ituri, DRC
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook