
Dodoma, Julai 29, 2025 – Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla, leo Julai 29, 2025 amezungumza na waandishi wa habari na kutoa taarifa rasmi kuhusu orodha ya wagombea wa nafasi za Ubunge walioteuliwa na chama hicho kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao.
Katika mkutano huo uliofanyika makao makuu ya chama, CPA Makalla alieleza kuwa uteuzi wa wagombea hao umezingatia vigezo mbalimbali ikiwemo uadilifu, uwezo wa kiuongozi, kukubalika kwa wananchi, na uzingatiaji wa maadili ya chama.
BONYEZA HAPA >>> ORODHA YA WAGOMBEA WA NAFASI ZA UBUNGE WALIOTEULIWA NA CHAMA
Amesema kuwa Kamati Kuu ya CCM Taifa ilipitia majina ya wagombea wote waliopita hatua za awali, ikiwa ni pamoja na mahojiano, uchambuzi wa taarifa zao, na mapendekezo ya vikao vya ngazi za chini kabla ya kufanya maamuzi ya mwisho.
CPA Makalla amewataka wagombea walioteuliwa kuwa na mshikamano, huku akisisitiza kuwa wote waliokosa nafasi hiyo bado wana nafasi ya kuendelea kulitumikia taifa kwa njia nyingine ndani ya chama.
“CCM itaendelea kuimarisha demokrasia ya ndani kwa kuhakikisha kila mwanachama anapata nafasi ya kushiriki kikamilifu katika shughuli za siasa kwa mujibu wa katiba ya chama chetu,” aliongeza Makalla.
Amesema orodha kamili ya majina ya wagombea walioteuliwa itabandikwa katika ofisi zote za CCM nchi nzima na pia kupatikana kupitia tovuti rasmi ya chama kwa ajili ya umma.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!