
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amepokea mkono wa pole kufuatia kifo cha kaka yake, Abbas Ali Mwinyi, kilichotokea jana tarehe 25 Septemba 2025.
Katika kuonesha mshikamano wa kitaifa kwa familia ya marehemu Abbas Mwinyi, viongozi mbalimbali wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, walifika kutoa mkono wa pole nyumbani kwa familia Bweleo, Mkoa wa Mjini Magharibi B.
Miongoni mwa walioungana na Rais Samia ni Naibu Waziri Mkuu, Mhe. Dotto Mashaka Biteko, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson Mwansasu, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Zuberi Ali Maulid, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Mhe. Dkt. Asha-Rose Migiro, pamoja na viongozi wengine mbalimbali.
Marehemu atasaliwa Masjid Jamia Zinjibar, Mazizini baada ya Sala ya Ijumaa, na kuzikwa Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja, leo tarehe 26 Septemba 2025.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!