Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Kilombero Sugar Yaadhimisha Miaka 23 ya Kutoa Mafunzo Kwa Viongozi Kupitia Mkutano wa Programu ya MIT 2025

  • 2
Scroll Down To Discover


Morogoro, Septemba 11, 2025 – Kampuni ya Sukari Kilombero imefanya Mkutano wa programu ya Managers in Training (MIT) 2025, kusherehekea miaka 23 tangu kuanzishwa kwa Programu hii ambao ni mahususi kwa ajili ya kulea na kutoa mafunzo kwa viongozi na wataalamu mbalimbali kwenye sekta ya sukari pamoja na Sekta nyingine nchini Tanzania.

Kwenye mkutano huo ambao ulihudhuriwa na viongozi wa serikali, viongozi wa kampuni mbalimbali na viongozi chipukizi, Bi. Diana Mwakitwange, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Kilombero Sugar, alisema kuwa programu hii ni uthibitisho tosha kuwa kampuni hiyo itaendelea kukuza na kulea viongozi wapya ambao wanatarajiwa kuendeleza sekta ya sukari nchini na nyingine kwa miaka mingi ijayo.

“Lengo la Programu hii sio tu kutoa mafunzo kwa wasimamizi wa kampuni mbalimbali lakini pia ni kutengeneza viongozi ambao wataongoza nchi hii kwa miaka na vizazi vijavyo” alisema

Akimwakilisha Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, ambaye kwenye mkutano huo aliwakilishwa na Kaimu Mkurugenzi wa TVET. Dkt. Mgaya aliipongeza Kilombero Sugar kwa uwekezaji wake wa kimkakati kwenye rasilimali watu:

“Programu hii sio tu kwamba inaonesha mafanikio ya Kilombero Sugar lakini pia ni hazina ya taifa. Kila mhitimu aliyepata mafunzo kutoka kwenye programu hii atakuwa ni mwenye ubunifu zaidi, ufanisi zaidi na ni fahari ya taifa.”

Aidha Mgaya alionyesha ni kwa jinsi gani programu hii ya kutoa mafunzo kwa uongozi, inavyoisaidia Tanzania kufanikiwa zaidi kwenye sekta viwanda, soko la ajira na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla.

Bw. Guy Williams, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Sukari Kilombero, akizungumzia kuhusu programu hiyo alisema:

“Uongozi sio kitu cha kurithi bali ni kitu ambacho kinafundishika. Kwa miaka 23, tumetoa mafunzo mameneja chipukizi zaidi ya 80 na wengi wao kwa sasa wameshika nafasi za juu kwenye kampuni mbalimbali.”

Alitoa wito kwa Wizara husika kuongeza kutoa ushirikiano ili kuziba pengo la ujuzi na maarifa kwenye sekta ya sukari kwa kutenga sehemu ya Kodi ya Maendeleo ya Ujuzi kuimarisha Taasisi ya Sukari ya Taifa (NSI).

Ambroce Heri, mshindi wa kwanza mwanafunzi wa kutoka Idara ya Kilimo cha Mashamba, alisema:

“Program hii umebadilisha mtazamo wangu sio tu kuhusu kilimo, bali pia kuhusu uongozi na jinsi ya kusaidia jamii.”

Mkutano huo pia uliangazia umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta ya sukari na taasisi za elimu. Hadi sasa, wahitimu 85 wamepitia wameshapata mafunzo w kutoka kwenye programu hiyo huku 27 kati ya hao wanafanya kazi kwenye kampuni ya Kilombero Sugar,

Aidha Wizara iliunga mkono juhudi za Kilombero Sugar za kuunganisha elimu ya nadharia na matumizi yake kwa vitendo kwenye sekta ya sukari nchini.

Mwishoni mwa mkutano, wadau waliahidi kuendeleza mpango programu hiyo, kuongeza ushirikiano na taasisi za elimu na kuangalia fani nyingine ambazo zinahitaji programu kama hizi.



Prev Post Dkt. Samia Ahahidi Miradi Mikubwa ya Maendeleo Kaliua, Tabora
Next Post Israeli yatishia kuwaua viongozi wa Hamas waliosalia Qatar
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook