
DAR-Huduma ya Mabasi Yaendayo Haraka (Mwendokasi) katika barabara ya Mbagala, ambayo awali ilitarajiwa kuanza Septemba 1, 2025 imesogezwa mbele kutokana na kutokamilika kwa miundombinu muhimu ikiwamo mageti janja na kituo cha kujazia gesi.
Akizungumzia kuhusu kutokamilika kwa miundombinu hiyo, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart),Dkt. Athuman Kihamia amesema, kuchelewa kuanza kwa huduma hiyo kunatokana na changamoto hizo licha ya mabasi kuwa tayari kwa ajili ya matumizi.
“Mabasi yamewasili, lakini hatutaweza kuanza kutoa huduma leo kama tulivyoahidiwa kwakuwa baadhi ya miundombinu haijakamilika. Mageti janja kwa ajili ya ukataji wa tiketi bado hayajafungwa na kituo cha kujazia gesi kilichopo kwenye karakana ya Mbagala nacho hakijakamilika.
“Hata hivyo, taarifa rasmi kuhusu maendeleo ya ujenzi huo tutaitoa baada ya wiki moja,”amesema Dk Kihamia .
Mabasi hayo 151 yaliwasili katika karakana ya Mbagala Rangi Tatu tarehe 29 Agosti, 2025 baada ya kutoka bandarini, shughuli iliyochukua takribani siku mbili.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!