Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Kesi ya Uhaini ya Tundu Lissu Kusikilizwa Mahakama Kuu Septemba 12

  • 6
Scroll Down To Discover

Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, imepangwa kusikilizwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, Septemba 12, 2025, katika hatua ya kusoma hoja za awali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, Septemba 1, 2025, na Wakili Gaston Shundo Garubindi, Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa CHADEMA, maandalizi yote ya awali yamekamilika. Taarifa hiyo pia imechapishwa kwenye ukurasa wa X wa Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho, Brenda Rupia.

Ikumbukwe kuwa Agosti 18, 2025, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliamua kupeleka shauri hilo Mahakama Kuu baada ya hatua zote za kisheria za awali kukamilika.



Prev Post MWISHOOO….AZAM WAGONGELEA MSUMARI KAULI YA SIMBA KWA FEI TOTO….
Next Post Uzinduzi Mabasi ya Mwendokasi Mbagala Wasogezwa Mbele
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook