Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Kulia), akipokea zawadi kutoka kwa Isack Kihwili Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Bima ya Amana wakati alipotembelea katika banda la bodi hiyo katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa Saba Saba yanayoendelea kwenye viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar er Salaam.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo, akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea katika banda la Bodi ya Bima ya Amana kwenye Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar er Salaam.
………
Na John Bukuku, Dar es Salaam
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo, ametembelea banda la Bodi ya Bima ya Amana (DIB) na kujionea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na bodi hiyo katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo, Dkt. Jafo alipata maelezo ya kina kuhusu majukumu na huduma zinazotolewa na DIB kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa bodi hiyo, Bw. Isack Kihwili.
Waziri huyo alipongeza kazi nzuri inayofanywa na DIB, hususan katika kuhakikisha utulivu wa sekta ya fedha kupitia ulinzi wa amana za wananchi katika taasisi za fedha.
“Niwahimize wananchi kuendelea kutumia huduma za kibenki kwa kujiamini, wakifahamu kuwa amana zao zinalindwa kupitia Bodi ya Bima ya Amana. Huu ni mfumo muhimu sana kwa usalama wa fedha na ustawi wa uchumi wetu,” alisema Dkt. Jafo.
DIB ina jukumu la kulinda amana za wateja wa taasisi za fedha zilizosajiliwa, na hivyo kuongeza imani kwa wananchi kutumia huduma za kifedha kwa usalama zaidi.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!