
Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa, Ndugu Othman Masoud, leo Agosti 21, 2025, anaongoza Kikao Maalum cha Kamati Kuu kinachoendelea hivi sasa katika Ukumbi wa Hakainde Hichilema, Jengo la Maalim Seif, Magomeni – Dar es Salaam.
Kikao hicho kimeitishwa mahsusi kwa ajili ya kufanya uteuzi wa mwisho wa wagombea wa ubunge na uwakilishi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Kwa mujibu wa viongozi wa chama hicho, kikao hiki kinachukuliwa kuwa ni hatua muhimu ya mwisho kabla ya wagombea hao kuridhishwa rasmi na kupokea baraka za chama kwa ajili ya kupeperusha bendera za ACT Wazalendo katika maeneo mbalimbali nchini.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!