

Dar es Salaam, Tanzania – 9 Julai 2025: Kampuni ya Acer Inc., moja ya vinara duniani katika suluhisho la kisasa za kompyuta, imetangaza upanuzi wake wa kimkakati katika soko la Afrika Mashariki. Acer inaleta safu kamili ya bidhaa zenye utendaji wa hali ya juu – kuanzia zile za kiwango cha mwanzo mpakai vifaa vyenye ubora wa kiwango cha juu – zilizobuniwa kukidhi mahitaji ya wafanyabiashara yanayobadilika kulingana na maendeleo, sekta ya elimu, wateja wa kawaida, na wachezaji michezo ya mtandaoni (gamers) katika ukanda huu. Hatua hii inaonyesha dhamira ya Acer kusaidia mabadiliko ya kidijitali Afrika Mashariki kupitia teknolojia ya kuaminika, salama, na bunifu.
“Lengo letu ni kuwezesha wafanyabiashara, shule na mahitaji ya nyumbani katika Afrika Mashariki kupitia teknolojia itakayoleta tija, ubunifu, burudani na uunganishwaji kiteknolojia,” amesema Grigory Nizovsky, Makamu wa Rais wa Acer kwa Kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika. “Kwa kuwa teknolojia inaendelea kubadilika kwa kasi, tumejikita katika kuondoa vizuizi vya mawasiliano baina ya watu ili kutatua changamoto kwa mahitaji mbalimbali. Tunajivunia kusaidia ukuaji huu kupitia suluhisho za kibiashara na elimu ambazo zitaboresha ufanisi na ubunifu.”
Acer imejijengea hadhi ya juu kama mshirika wa kuaminika katika sekta ya elimu kwa kutoa vifaa vya kutegemewa, rahisi kutumia, na suluhisho zinazowawezesha wanafunzi na walimu. Kupitia bidhaa zake mbalimbali kama vile Chromebook, kompyuta mpakato na teknolojia za madarasani, Acer inaunga mkono mazingira ya kujifunza kidijitali mashuleni na vyuoni kote ulimwenguni. Sekta ya elimu ni kipaumbele muhimu kwa Acer kwa kuwa inachochea ukuaji wa muda mrefu, kukuza ujumuishaji wa kidijitali, na kujenga jamii bora yenye kujiandaa kwa siku zijazo – jambo linaloendana na kaulimbiu ya kampuni: “kuondoa vizingiti kupitia teknolojia”, hususani katika elimu.
Bidhaa mpya zitakazopatikana katika Ukanda huu zimegawanywa katika makundi matatu makuu: Biashara na Elimu, Watumiaji wa Kawaida, na Michezo ya Kielektroniki au Mtandaoni (Gaming). Kila kundi limetengenezewa bidhaa mahsusi kusaidia mahitaji yanayokua ya wafanyabiashara, wanafunzi, familia na wapenzi wa michezo ya kidijitali.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!