

MAMLAKA ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), imewataka wawekezaji kuja kuwekeza katika masuala ya Nishati Safi kutokana na kuwepo mikakati imara, mazingira wezeshi, amani na utulivu inayotoa fursa kwa maendeleo ya kiuchumi.
Akizungumza na wanahabari mapema leo, Julai,9,2025, jijini Dar-es-Salaam Mkurugenzi Mkuu kutoka Pura,Mhandisi Charles .Sangweni amesema kuwa kuwepo kwa mazingira wezeshi, amani na utulivu shughuli za uzalishaji katika mkondo wa Juu wa Petrol kwenye nyanja ya ajira imeongezeka kutoka asilimia 55 hadi 85.
“Tumekuwa tukishiriki Katika Maonyesho haya mwaka 2017 na mwaka huu yamekuwa mazuri kutokana na kuendeshwa kidigitali na tutaendelea kushiriki kwa mafanikio makubwa na kwa mwaka huu tumepata maswali mazito kutoka kwa wananchi wanaofika kutembelea banda letu kuhusu nishati safi na tumewajibu kwa mapana na ninaamini wameridhika,” amesema.
“Tunamshukuru Mhe Rais,Dkt,Samia Suhuhu Hassan kwani amefanya kazi kubwa katika uwekezaji katika mamlaka hii kwani kuanzia mishahara na uwepo wa mazingira wezeshi na rafiki kwa wawekezaji, hivyo ni wakati wao wawekezaji kuitumia nafasi hiyo kuja kuwekeza hapa nchini hususan katika Nishati Safi,” amesema.
“Kati ya kampuni 10 zinazoshughulika na utafutaji mafuta na gesi sita ni za kitanzania na hiyo inatokana na kuwepo mpango wa mkakati wa kuhakikisha vyuo vya Tanzania zifundisha kozi za mafuta na gesi na wahitimu wanapomaliza masomo yanaingia moja kwa moja kufanya shughuli hizo.
“Kwa sasa tupo katika mchakato wa kuchimba visima vitatu vya gesi asilia mkoani Mtwara unaotarajia kuanza Novemba mwaka huu unaotarajiwa kuongeza uzalishaji wa gesi asilia kutoka kitalu cha Mnazi Bay kwa zaidi ya ujazo wa milioni 30 kwa siku jambo ambalo litakuwa ni mafanikio ya kujivunia,”amesema Mhandisi Sangweni .
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!