Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Bosi Azam FC Afungukia Kuhusu Fei Toto

  • 42
Scroll Down To Discover

FEISAL Salum, Fei Toto kiungo wa Azam FC

FEISAL Salum, Fei Toto kiungo wa Azam FC ambaye ni namba moja kwenye pasi za mwisho za mabao ndani ya Ligi Kuu Bara ambayo ni namba nne kwa ubora jina lake limekuwa likitajwa kuwa katika rada za Simba.

Kiungo huyo aliibuka ndani ya Azam FC akitokea Yanga ambapo kwa sasa amekuwa ni chaguo la kwanza kwenye viunga vya Azam Complex akiwa ametoa jumla ya pasi 12 za mabao kati ya 36 yalyofungwa na timu hiyo.

Nafasi ya tatu kwenye msimamo ipo baada ya kucheza mechi 23 kibindoni ina pointi 48 vinara ni Yanga wenye pointi 58 na Simba inayotajwa kuwa kwenye hesabu za kuisaka saini ya Fei Toto ni nafasi ya pili na pointi 57.

Ikumbukwe kwamba baada ya mchezo wa Mzizima Dabi uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao uliposoma Simba 2-2 Azam FC, Fei Toto alivaa uzi wa Simba walipobadilishana na mchezaji Shomari Kapombe jambo ambalo liliongeza gumzo.

Kuhusu Sakata hilo, Mkuu wa Idara ya Habari ndani ya Azam FC, Zakazakazi amesema kuwa ilikuwa ni gumzo kubwa kwa Fei Toto kutokana na thamani yake kuwa kubwa jambo ambalo linaleta gumzo.

“Kwa Fei Toto kuvaa jezi ya Simba baada ya mchezo hiyo ilikuwa ni stori kubwa kutokana na thamani ya mchezaji, akifanya kitu chochote kinapoteza yote yaliyokuwa yanafanyika awali kutokana na uwezo wake ila bado atabaki kuwa mchezaji wetu.”



Prev Post Walimu mbaroni kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka 10
Next Post Yanga Yavunja Rekodi Za Simba Ndani Ya Dakika 90
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook