Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Makalla: Rais Samia Aagiza Uteuzi wa CCM Ufanyike kwa Haki – Video

  • 36
Scroll Down To Discover

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) – Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla.

Dar es Salaam, Julai 3, 2025 – Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amevitaka vikao vya uchujaji na uteuzi wa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho kutenda haki, huku haki hiyo ikionekana wazi ikitendeka.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) – Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla amesema:

“Mwenyekiti wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan anavitaka vikao vya uchujaji na uteuzi vitende haki, na haki hiyo ionekane kwa macho ya wote. Visionee watu, tusitengeneze fitna wala majungu dhidi ya wagombea. Tusionee mtu yeyote bali tumteue anayeendana na maadili na sifa stahiki za CCM.”

Makalla amesema kuwa chama kinaelekea kwenye uchaguzi kikiwa na orodha ndefu ya mafanikio yaliyopatikana chini ya Ilani ya CCM, hivyo ni muhimu kuwa na wagombea bora watakaoweza kuyasimamia na kuyatetea mafanikio hayo kwa ufanisi mkubwa.

“Haya mafanikio tutayazungumza kwenye kampeni, lakini tutayabeba vyema ikiwa tutakuwa na wagombea wenye mvuto na sifa. Haki ikitendeka kwenye uchujaji, tutapata wagombea wazuri, na malalamiko yatapungua,” alisisitiza.

Makalla ameongeza kuwa kesho Julai 4, 2025, vikao vya uchujaji wa wagombea vinaanza rasmi katika ngazi ya kata. Baada ya hapo, mchakato huo utaendelea katika ngazi za wilaya, mikoa, na hatimaye kufikia Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ambayo itatoa uamuzi wa mwisho wa majina ya wagombea wa nafasi za udiwani, ubunge na uwakilishi.

“Kila kikao kinapaswa kufanya kazi yake kwa uadilifu. Tukifanya hivyo, tutajenga imani kwa wanachama wetu na kwa Watanzania wote,” alisema Makalla.

Ametumia fursa hiyo kuwataka wanachama wa CCM kuwa watulivu na kuviamini vikao vya chama, akisema kuwa Mwenyekiti wao ameweka msisitizo wa dhati kuhakikisha hakuna upendeleo wala uonevu katika mchakato wa uteuzi wa wagombea.



Prev Post UDOM Wabuni Roketi ya Kupeleka Vitu Angani
Next Post CCM Yamsifu Majaliwa Kwa Uamuzi Wake Wa Kutogombea Ubunge – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook