Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

UDOM Wabuni Roketi ya Kupeleka Vitu Angani

  • 8
Scroll Down To Discover

Mhadhiri wa UDOM, Dkt. Phiano Tumaini akielezea jinsi roketi hiyo inavyofanyakazi.

Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) katika kinachoonekana kupiga hatua katika masuala ya sayansi na teknolojia wamebuni roketi yenye uwezo wa kusafiri umbali mrefu angani na kupeleka vitu mbalimbali.

Akizungumza na mwanahabari wa Global TV, Neema Adrian.

Akizungumza na wanahabari wetu kwenye maonesho ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam mhadhiri wa chuo hicho, Dkt. Phiano Tumaini, amesema roketi ni mafanikio ya masomo ya sayanasi yanayotolewa na chuo hicho.

Amesema roketi ni kama roketi nyingine unazozifahamu ambapo kazi yake kubwa ni kutuma vitu angani pamoja kubeba vitu kama makombora, satellite na vinginevyo na kuendelea kusema;

“Ubunifu ulituchukua miaka kadhaa kuiboresha kwa maana awali ilikuwa unaweza kuituma angani lakini ilikuwa haindi umbali mrefu na wakati mweingine ilikuwa ikipoteza mwelekeo iwapo angani lakini kwa sasa haina changamoto tena”.

Tunawakaribisha wadau mbalimbali waje kwenye banda letu lililopo Viwanja vya Sabasaba ili wajionee mambo mambo mbalimbali ikiwemo mafanikio makubwa ya kisayansi na teknolojia. HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS NA NEEMA ADRIAN /GPL



Prev Post Waziri Paramagamba Kabudi Alivyofika Banda la NIC Sabasaba Kujionea
Next Post Makalla: Rais Samia Aagiza Uteuzi wa CCM Ufanyike kwa Haki – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook