

Dar es Salaam 3 Julai 2025: Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuwa miongoni mwa mashirika yanayostahili kupewa miradi mbalimbali ya kitaifa ni pamoja na Shirika la Bima Taifa (NIC) kwani limekuwa likionesha uwezo mkubwa pindi wanapokuwa wakitekeleza miradi hiyo.
Prof. Kabudi amebainisha hayo alipotembelea Banda la Shirika hilo, kwenye maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba, yanayofanyika Jijini Dar es Salaam.
Amesema NIC kupewa fursa hiyo so suala la upendeleo bali wanastahili kwa uwezo walionao nakwamba wanastahili.
Aidha, ameloshukuru Shirika hilo kwa kuungamkono kwa vitendo sekta ya michezo kwa kudhamini Klabu zote zinazoshiriki Mapinduzi Cup pamoja na timu za Pamba na Yanga, akisema kuwa huo ni mfano wa kuigwa na mashirika mengine.
“Nashukuru sana kwa kushajiisha sekta ya michezo na kuwa wadhamini wa Klabu zote ya Mapinduzi Cup, Pamba Cup na Yanga Fc hii ni moja ya kuonesha ni namna gani mpo vizuri hata katika sekta ya michezo,” alisema
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa NIC, Karim Meshack, amesema kuwa Shirika hilo, ina dhamira ya dhati katika kuhakikisha inaunga mkono juhudi za Serikali katika kukuza sekta ya michezo nchini. NIC inaketeleza miradi mbalimbali katika sekta ya michezo ikiwemo ujenzi wa Viwanja.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!