

Jeshi la Mali limesema limewaua wapiganaji 80 wa Al-Qaeda waliovamia vituo vya kijeshi kwa mashambulizi ya ghafla katika miji saba ya kati na magharibi mwa nchi, karibu na mipaka ya Senegal na Mauritania.
Katika taarifa maalum kupitia runinga ya jeshi, viongozi wa kijeshi walisema mashambulizi hayo yalibeba alama za kundi la kigaidi la Jama’at Nusrat al-Islam wal-Muslimin (JNIM), ambalo linahusiana na Al-Qaeda na limekiri kuhusika, likidai pia kudhibiti kambi tatu za kijeshi.
Tukio hili linajiri wakati Mali inazidi kukabiliwa na wimbi la uasi wa makundi ya Kiislamu wenye mafungamano na Islamic State pamoja na Al-Qaeda.

Mwezi Mei, Mkuu wa Jeshi la Marekani barani Afrika (AFRICOM), Jenerali Michael Langley, alionya kuwa eneo la Sahel sasa limegeuka kuwa “kitovu cha ugaidi duniani”, huku magaidi wakilenga kuenea hadi fukwe za Afrika Magharibi ili kuongeza mapato kupitia biashara haramu ya binadamu, silaha na magendo.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!