

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa hatagombea tena ubunge wa Jimbo la Ruangwa katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025, baada ya kuliongoza jimbo hilo kwa miaka 15 mfululizo.
Taarifa za Majaliwa kutogombea tena, zimetolewa na Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ruangwa, Mkoa wa Lindi, Abbas Makweta ambaye amesema Majaliwa amefika kwenye ofisi hizo asubuhi ya leo, Julai 2, 2025 na kueleza kuwa hatagombea tena ubunge.
Zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu ndani ya CCM za udiwani na ubunge linatarajiwa kufungwa leo Jumatano, Julai 2, 2025 majira ya saa 10:00 jioni.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!