

MTIA NIA na Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Kinondoni Iddi Azzan amechukua fomu kuwania nafasi ya Ubunge katika Jimbo hilo, kwa ajili ya kwenda kuyatimizia wananchi mambo ambayo bado yameonekana kuwa kikwazo kwao.
Mtia nia Azzan alisema nayo jana Jijini Da es Salaam, wakati alipokuwa akichukuwa fomu kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Kinondoni ambapo fomu hizo zimetolewa kwenye Ofisi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) chini ya Kaimu Katibu wa hama hicho Amos Richard.

Iddi Azzan aliwahi kuwa Mbunge katika Jimbo hilo toka 2025 -2015 ambapo alisema yapo mambo ambayo aliwahi kuyafanya wakati huo alivyokuwa Mbunge na kipindi kilichofuata aliamini mambo hayo yangeweza kufanyiwa kazi kwa haraka ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya barabara za ndani, hivyo mambo hayo ameshangzwa hayakufanyiwa kazi hadi Sasa, hivyo ameona achukue fomu kwenda kuwatekelezea wananchi jambo lao.
“Ni kweli nilishawahi kuwa Mbunge kwenye Jimbo la Kinondoni miaka ya 2025-2015 na nilijitahidi kutimiza changamoto za wananchi,, lkn pia nimeamua kurudi tena kwa mara nyingine ili kutimiza jambo lao na mimi wananchi wa Jimbo hili wananiamini na mimi nawaamini”alisema Azzan.
katika hatua nyingine, Azzan amesema Chama cha Mapinduzi CCM kimesema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, hakishindanishi wagombea matajri na watoa rushwa, bali wanaotakiwa ni viongozi waadilifu na wenye kuleta maendeleo kwa wananchi.
Mtia nia Azzan alisema kauli ya Chama inapaswa kuheshimika kutokana na ukumbwa wa Chama hicho na viongozi wake waliyopo ndani ya Chama.
“Chama chetu kimeweka utaratibu mzuri sana ya sisi wagombea kuwa makini na kujiepusha na vitendo vya kutoa ama kupokea rushwa kipindi hiki cha uchaguzi na utaratibu huo umeelekezwa kwenye kanuni za uchaguzi zipo wazi na pia Chama hakitafuti tajiri bali kinatafuta mgombea anayekubalija ndani na nje ya Chama”alisema Azzan.
Aidha ameongeza kwa kusema anaimani na Chama cha Mapinduzi kufanyamchakato wake mzuri wa kurejesha majina matatu, hivyo anaimani kwamba jina lake likirudi sasa atakuwa tayari kuwatumikia wananchi wake.
Zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za ubunge katika Wilaya ya Kinondoni imechukua sura ya pili tangy pazia hilo lilipofunguliwa juzi Juni 28 mwaka huu na mwisho wa zoezi hilo ni Juni 29 mwaka huu.
Naye Mtina nia wa nafasi ya udiwani viti maalum Jimbo la Kinondoni Daines Masokola amechukua fomu kuwania nafasi hiyo na huku akisema Chama cheke CCM kikimpitisha jina lake basi anaweza kuwatumikia wananchi wake kwa ufanisi.
Mtia nia huyo ambaye pia ni Katibu wa Elimu, Malezi, Michezo na Afya (EMMA) kutoka Kata ya Hananasifu amesema anaimani na Chama chake kwani kitakwenda kutenda haki kwa wagombea waliyotia nia kuomba nafasi mbalimbali kwenye Serikali.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!