Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Kazi ipo! Hamisi Slim wa Equator Grill Achukua Fomu Kuwania Udiwani

  • 46
Scroll Down To Discover

Hamisi Slim (kushoto) akipokea fomu kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Kata ya Kijichi, Magdalena Komba.

Dar es Salaam 28 Juni 2025: Kazi ipo! Hivyo ndivyo unaweza kusema kufuatia makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kufungua dirisha la uchukuaji na urudishaji wa fomu za kutia nia ya kugombea nafasi za ubunge na madiwani kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Miongoni mwa watia nia hao ni kada wa CCM wa miaka mingi, Hamisi Slim ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Temeke, Dar amechukua fomu ya kutia ya kugombea udiwani Kata ya Kijichi Dar.

Pamoja mambo mengine Slim alijipatia umaarufu mkubwa wilayani Temeke kufuatia Ukumbi wake wa Equator Grill kutumika bure siku zote katika shughuli zote za kichama na serikali ambapo zimebidi kufanyika hapo.

Sifa kubwa na mambo mengi aliyowatendea Wana Temeke katika nafasi ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi huenda ndiyo iliyomhasisha kutia nia ya kugombea udiwani huo. HABARI/PICHA NA ISSA MNALLY/ GPL



Prev Post Kenya: 16 Wameuawa Kwenye Maandamano Kenya
Next Post Furaha Dominic Aliyekubalika na Wajumbe Kawe Airudia Tena Kawe Yake
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook