Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Kenya: 16 Wameuawa Kwenye Maandamano Kenya

  • 48
Scroll Down To Discover


Watu kumi na sita wamdaiwa kuuawa na polisi wakati wa maandamano ya kitaifa dhidi ya serikali nchini Kenya siku ya Jumatano.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Amnesty Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty Kenya, vifo hivyo vinatokea mwaka mmoja baada ya maandamano ya vurugu dhidi ya muswada wa kodi ambapo zaidi ya watu 60 walidaiwa kuuawa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Amnesty Kenya, Irungu Houghton, amesema kuwa baadhi ya waandamanaji walikabiliana na polisi, huku watu 16 wamethibitishwa kufariki dunia.
Houghton amesema takwimu hizo zilithibitishwa kwa pamoja na Shirika la Amnesty Kenya pamoja na Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu (KNCHR).

KNCHR, taasisi ya serikali, awali iliripoti kuwa watu wanane walifariki dunia kutokana na majeraha ya risasi na zaidi ya watu 400 walijeruhiwa, wakiwemo waandamanaji, maafisa wa polisi na waandishi wa habari.

Katika taarifa iliyotolewa kupitia akaunti rasmi ya mtandao wa kijamii wa X, KNCHR ilieleza kuwepo kwa madai ya matumizi ya nguvu kupita kiasi ya polisi, ikiwemo matumizi ya risasi za mpira, risasi za moto na maji ya kuwasha.
Msemaji wa polisi nchini Kenya, Muchiri Nyaga, alikataa kutoa maoni kuhusu taarifa zilizotolewa na Amnesty Kenya na KNCHR.

Kwa upande mwengine Taasisi ya Usimamizi Huru wa Polisi (IPOA), ambayo pia inafadhiliwa na serikali, ilisema kuwa watu wasiopungua 61 walikamatwa wakati wa maandamano hayo.

STORI NA ELVAN STAMBULI, GPL.



Prev Post Boti ya Uokozi Yawashtua Mwanza! Wananchi Waipokea kwa Shangwe – Video
Next Post Kazi ipo! Hamisi Slim wa Equator Grill Achukua Fomu Kuwania Udiwani
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook