
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemteua Gerva Lyenda kuwa Mkuu wa Idara ya Habari wa Kurugenzi ya Habari na Uenezi ya chama hicho kuanzia Jumatatu, tarehe 25 Agosti 2025.
Taarifa ya uteuzi huo imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho, Brenda Rupia, ambaye amesema uteuzi wa Lyenda unalenga kuimarisha mikakati ya chama katika eneo la mawasiliano, hususan kuelekea katika kipindi cha maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa 2025.
“Uongozi wa chama una imani kuwa Bw. Lyenda atatekeleza majukumu yake kwa weledi, ubunifu na ufanisi, ili kuhakikisha taarifa na mawasiliano ya chama yanafika kwa wanachama na umma kwa ujumla kwa wakati na kwa usahihi,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Gerva Lyenda anachukua nafasi hiyo katika kipindi ambacho chama kinapanua jitihada zake za kuimarisha mtandao wa mawasiliano, hususan kupitia vyombo vya habari na majukwaa ya kidijitali.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!