

Kama kuna kitu kilichowaumiza watu wa Jimbo la Kawe haswa wajumbe waliompitisha kugombea katika Uchaguzi Mkuu wa 2020 ni kumchagua kwa kura za kutosha kuwaongoza mtia nia ya Ubunge Kijana Msomi na Kada wa Chama cha Mapinduzi, Furaha Dominic ambaye hata hivyo jina lake lilikatwa kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi.

Katika kuonekana kutaka kuwarejeshea furaha yao wajumbe hao na wakazi wa Jimbo la Kawe kwa ujumla kada huyo wa Chama cha Mapinduzi CCM mwaka huu amerejea tena na kutia nia ya kuligombea jimbo hilo lililokuwa likishikiliwa na Mchungaji Josephat Gwajima aliyewekwa nafasi hiyo akiwa nafasi ya tatu katika kura za maoni ya wajumbe baada ya jina la Furaha Dominic lililokuwa namba moja kukatwa.

Mwanahabari wetu alimshuhudia Furaha akirejesha fomu ya kutia nia ya kugombea jimbo hilo katika Ofisi za CCM Wilaya ya Kinondoni huku akionekana mwenye furaha tele na kuwachangamkia watia nia wenzake huenda ni baada ya kuwachungulia anaopambana nao.

Furaha ni kama anaurejea mtihani ambao alishawahi kuufaulu. Watia nia wengine wanaendelea kwenda kuchukua na kurudisha fomu za kuligombea jimbo hilo. HABARI/PICHA :RICHARD BUKOS, GPL
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!