
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendeleza juhudi za kuboresha usalama wa usafiri wa majini nchini kwa kuwakabidhi wakazi wa Mkoa wa Mwanza boti ya kisasa ya uokozi.
Wananchi wa mkoa huo wamepokea kwa furaha hatua hiyo ya serikali, wakisema kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na ukosefu wa boti ya uokozi — jambo ambalo limechangia vifo vya wananchi wakati wa ajali za majini. Wameeleza kuwa hatua hiyo ni ishara ya dhahiri kuwa serikali ya awamu ya sita inaweka maisha ya wananchi mbele.
Benadeta Mohamed, mkazi wa Mwanza, alieleza hisia zake kwa kusema:
“Sisi hatumdai Mama (Rais Samia), bali yeye ndiye anatudai kura ya ‘Ndiyo’ ili aendelee kuiongoza nchi kwa miaka mitano tena.”
Wananchi wengine pia wamepongeza hatua hiyo wakisema inathibitisha dhamira ya dhati ya Rais Samia katika kuimarisha miundombinu ya usalama Ziwa Victoria ambako usafiri wa majini ni sehemu ya maisha ya kila siku.
Boti hiyo ya uokozi inatarajiwa kusaidia katika shughuli za haraka za kuokoa maisha pindi ajali zinapotokea, pamoja na kusaidia ufuatiliaji wa usalama wa wavuvi na abiria kwenye maeneo ya ziwa.
Hatua hii ni mwendelezo wa mikakati ya serikali ya kuhakikisha kuwa usafiri wa majini, ambao ni kiungo muhimu kwa uchumi na maisha ya Watanzania, unakuwa salama na wa kuaminika.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!