Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Kampuni ya Meridianbet Yasaidia Usafi wa Mazingira Kinondoni

  • 12
Scroll Down To Discover

Kampuni kubwa ya ubashiri Tanzania, Meridianbet leo hii iliamua kufunga safari moja kwa moja mpaka mtaa wa Mpakni Kinondoni B na kugawa mapipa ya taka kwa lengo la kuwezesha ukusanyaji mzuri wa taka na kudumisha mazingira safi.

Katika tukio hilo la kutoa mapipa hayo ya taka, Meridianbet ilisema kuwa vifaa hivyo vina lengo la kusaidia ukusanyaji bora wa taka, kuimarisha usafi wa mitaa, na kuongeza usalama kwa wale wanaojihusisha na kazi za usafi hususani wakati wa alfajiri na jioni.

Hatua hii imepokelewa kwa shukrani kubwa kutoka kwa viongozi wa serikali za mitaa pamoja na wananchi wa Kinondoni B, ambao wameeleza kuwa msaada huu umefika wakati muafaka ambapo suala la usafi limekuwa changamoto kwa jamii nyingi mijini.

Meridianbet alisema kuwa, “Tunaamini kuwa usafi ni nguzo muhimu ya afya na maendeleo. Kwa kugawa mapipa haya ya taka, tunalenga kusaidia Ofisi ya Serikali ya Mtaa kufanya usambazaji sahihi kwa taasisi zinazowahudumia watu wengi kila siku  hasa watoto mashuleni na wagonjwa hospitalini.”

Kwa upande wa Kinondoni kupitia Mwenyekiti wao wa Mtaa wa Mpakani B alifurahia sana ujio wa Meridianbet na akasema kuwa,  “Tunafurahia kuona taasisi kama Meridianbet zikijitokeza kusaidia jamii yetu. Hii ni hatua nzuri ya kuimarisha mazingira yetu na ni mfano wa kuigwa na wengine.”

Dhamira ya CSR ya Meridianbet kwa mwaka huu imejikita katika kaulimbiu ya “Usafi ni Afya, na Afya ni Maisha”. Hii ni hatua ya kuunga mkono juhudi za kitaifa na kimataifa katika kutunza mazingira, kupambana na magonjwa yanayosababishwa na uchafu, na kujenga jamii zenye afya bora. Kwa kufanya hivi, Meridianbet haijajikita tu kwenye kusaidia kifedha au kimali, bali pia inawekeza katika kuibadilisha fikra na mitazamo ya jamii kuhusu uwajibikaji wa pamoja kwa maslahi ya wote.

Ukiachana na hilo, Meridianbet inakuambia kuwa kuna michezo kibao ya kukupatia mkwanja leo kama vile Poker, Keno, Roulette, Aviator, Superheli hivyo ingia na ukusanye maokoto zaidi na zaidi. Pia ongeza maokoto yako kwa kubashiri michezo mbalimbali yenye ODDS KUBWA. PIGA *149*10# AU tembelea tovuti yao meridianbet.co.tz

Meridianbet imeendelea kuwa mdau mkubwa wa maendeleo ya jamii nchini Tanzania kupitia miradi mbalimbali inayogusa sekta za elimu, afya, michezo, na mazingira. Ugawaji huu wa dustbins ni mwendelezo wa dhamira ya kampuni hiyo ya kuwa sehemu ya suluhisho la changamoto zinazowakabili wananchi wa kawaida. 



Prev Post Baada ya kusumbuka sana, dawa hii imenisaidia kubeba ujauzito
Next Post Majaliwa Aagiza Usimamiaji Na Udhibiti Wa Ubora Wa Elimu
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook