Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Iran Yaanzisha Mashambulizi ya Makombora Dhidi ya Israel – Video

  • 9
Scroll Down To Discover

Katika tukio la kushtua dunia, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilirusha makombora mawili kuelekea Israel alfajiri ya Jumatano, Juni 18, 2025.

Shambulio hilo, lililofanywa kupitia mashambulizi mawili tofauti ya makombora, linatajwa kuwa sehemu ya operesheni inayojulikana kama “Ahadi ya Ukweli 3 (Honest Promise 3)”, iliyotangazwa na Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).

Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, alitoa kauli kali akisema “vita vimeanza” na kuwataka Wairani “wasioneshe huruma” kwa Waisraeli.

Mashambulizi ya kwanza yalianza saa 12:40 alfajiri kwa saa za Israel, ambapo takriban makombora 15 yalirusha na kusababisha milio ya ving’ora ya tahadhari katika maeneo mengi ya Israel, ikiwemo miji mikuu na vitongoji vyake.

Takriban dakika 40 baadaye, mashambulizi ya pili ya takriban makombora 10 yalifuata, na kusababisha hofu katika jamii za Kati mwa Israel pamoja na maeneo ya Ukanda wa Magharibi (West Bank).

Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) lilikuwa tayari limewatahadharisha raia wake dakika chache kabla ya mashambulizi, likiwaagiza kuingia mafichoni. Baada ya kila mashambulizi, IDF ilitangaza kuwa hali imetulia na ilikuwa salama kwa watu kuondoka kwenye hifadhi.



Prev Post Waziri Mkuu Atoa Wito kwa Watafiti “Tafiti Zilete Tija kwa Wananchi”
Next Post Puma Energy Tanzania Yashiriki Kongamano Kukuza Ushirikishwaji Watanzania Sekta ya Madini.
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook