

Kila nilipoamka asubuhi nilihisi kama dunia imenigeuka, nikiona mashinikizo ya watu waliotaka kulipwa pesa zao bila huruma. Nilipoteza heshima, marafiki waliniepuka, na hata ndugu walinigeuka wakisema mimi ni mzigo. Nilipokuwa nikitembea mtaani nilihisi macho ya watu yakinitazama kwa kejeli, kana kwamba walijua siri yangu ya kufilisika.
Kila hatua niliyopiga ilikuwa ni ya taabu. Nilijaribu kuuza mali ndogo ndogo niliyo nayo ili kufidia deni, lakini bado zilikuwa haziwezi kulingana na mzigo nilioubeba. Nilipoona mashine yangu ya biashara ikichukuliwa kama dhamana, moyo wangu ulivunjika.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!