Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Rais Mstaafu Kikwete Awataka Wanachama Kupuuza Maneno ya Upotoshaji – Video

  • 8
Scroll Down To Discover

Dar es Salaam, Agosti 28, 2025 – Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amewataka wananchi na wanachama wa CCM kupuuza maneno yanayodai kuwa taratibu za kumpitisha Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea urais wa chama hicho zimekiukwa.

Akihutubia katika uzinduzi wa kampeni za CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Dkt. Kikwete alisema taratibu zilizotumika kumuidhinisha Rais Samia ndizo hizo hizo zilizotumika kuwapitisha wagombea wote wa urais wa CCM tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi.

“Hakuna Kipya, Hakuna Kilichokiukwa”

Kikwete alieleza kuwa ni jambo la kushangaza kwa watu waliokuwepo ndani ya chama kipindi cha kupitishwa wagombea wa zamani sasa kudai kwamba taratibu zimevunjwa.

“Kulikuwepo na maneno ama vijineno eti utaratibu umekiukwa, na mimi nililaumiwa kwa jinsi nilivyosema pale kwenye mkutano mkuu. Lakini nasema wazi: waliokuwa wanayasema hayo ama hawajui utaratibu wa chama chetu, au wanajifanya kusahau,” alisema.

Mfumo wa Vyama Vingi na Utaratibu wa CCM

Dkt. Kikwete alifafanua kuwa tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi, CCM imejiwekea utaratibu maalum kwamba Rais aliyepo madarakani anapomaliza muhula wake wa kwanza na kutaka kuendelea muhula wa pili, hupitishwa bila kupingwa.

“Ndivyo ilivyokuwa kwa Rais Benjamin Mkapa, ndivyo ilivyokuwa kwangu, na ndivyo ilivyokuwa kwa Rais John Magufuli. Kwa nini leo tunasikia kelele za kutaka tofauti kwa Rais Samia? Sababu yake nini? Mbona haya hatukuyasikia kwa Mkapa, wala kwa Kikwete, wala kwa Magufuli?” alihoji kwa msisitizo.

Msimamo wa Viongozi Wastaafu

Kauli ya Kikwete inakuja ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono uhalali wa mchakato uliomuidhinisha Rais Samia kuwa mgombea wa CCM, hatua iliyozua mijadala katika mitandao ya kijamii na baadhi ya vikao vya kisiasa.

Kwa mujibu wa Kikwete, mjadala huo hauna mashiko kwa kuwa historia ya chama hicho imekuwa ikifuata taratibu hizo kwa ufanisi bila upendeleo.



Prev Post CCM Yazindua Kampeni Kawe, Samia Atangaza Ajenda Mpya – (Video +Picha)
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook