Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mbeto: Jussa fanya Siasa safi, acha kumkashifu Mwalimu Nyerere

  • 30
Scroll Down To Discover

Chama Cha Mapinduzi kimetamka Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendoakome kumwita Marehemu Baba Taifa Mwalimu Julius Nyerere alikuwa Kiongozi mshenzi wakati amelitumikia Taifa miaka 23 kwa Uzalendo na Uaminifu.

Pia chama hicho kimemkanya Jussa asiulinganishe upeo wake na Mwalimu Nyerere kwani hata Hayati Maalim Self Sharif Hamad hakuwahi kutoa kashfa dhidi ya Marehemu Mwalimu Nyerere.

Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo , Khamis Mbeto Khamis ameeleza hayo akimuonya Jussa asimkashifu na kulidhihaki jina la Baba wa Taifa ambaye bado anaheshimika duniani .

Mbeto alisema kama Jussa ni hodari wa kutukana matusi viongozi na kuwakebehi , kwanza aanze kumtukana Marehemu Maalim Seif ambaye pia ametangulia mbele ya haki.

Alisema inashangaza kumsikia Makamu huyo Mwenyekiti wa ACT , akimwita Mwalimu Nyerere ni mshenzi na wenzake walioazimia kumfukuza CCM Maalim Seif na wenzake sita Mwaka 1987.

“Kinachofanywa na Jussa katika majukwaa ya Siasa si katika Siasa safi na uungwana adilifu .Siasa za matusi na kashfa hazikubaliki katika Taifa la kiuungwana kama Tanzania ” Alisema

Mbeto amedai Jussa akiwa katika kikao cha ndani cha ACT Wazalendo,huko Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Mkoa wa Kaskazini Unguja , pamoja na maneno ya kejeli amelidhalilisha jina,utu na hadhi ya Marehemu Mwalimu Nyerere

Hata hivyo, Mwenezi huyo alisema Jussa alikwenda mbali na kuwaita Viongozi wote wa CCM ni majahili ,wezi wa kura ,hawamuhofu mungu pia hawana imani za dini .

Hivyo basi, Mbeto alizungumzia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba Mwaka huu, alisema hauna kisasi na yeyote badala yake wananchi wanajiandaa kutimiza matakwa ya Katiba ,sheria na demokrasia .

Alisema matamshi ya Jussa katika kikao hicho, si kwamba tu yanaweza kupandikiza hasama na chuki , lakini pia ameitumia Dini kuwadhalilisha wenzake katika ulingo wa Siasa.

“Jussa ajue kuwa Wazanzibari hawaiishi kwa vonyongo,visasi na chuki . Kuwaita wenzake majahili , hawana imani ya dini ni wazi amekusudia kupandikiza na kueneza chuki” Alisema Mbeto

Katibu Mwenezi huyo alimtaka Jussa kuacha kumkejeli Mwalimu Nyerere kwani licha kuleta uhuru,kuasisi Taifa, Muungano ,amejenga misingi ilioleta Amani, Umoja wa Kitaifa na Mshikamano uliopo



Prev Post Rais Samia Apokea Gawio Na Michango Kutoka Kwa Taasisi Na Mashirika Ya Umma (Picha +Video)
Next Post Mbeto: Jussa fanya Siasa safi, acha kumkashifu Mwalimu Nyerere
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook