Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

28 WAITWA TAIFA STARS….SAMATTA AOMBA POOO….MZINZE, MUDATHIR MHHH…..

  • 34
Scroll Down To Discover

KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Hemed Suleiman ‘Morocco’, ametaja kikosi cha nyota 28 kwa ajili ya kujiwinda na mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’, itakayopigwa Juni 6 mwaka huu nchini Afrika Kusini.

Mbali na mechi hiyo dhidi ya Bafana Bafana iliyomaliza nafasi ya tatu kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) iliyofanyika Ivory Coast 2023, Stars inajiwinda na mashindano ya Baraza la Vyama vya Soka Kusini mwa Afrika (COSAFA).

Katika michuano hiyo ya COSAFA, Stars itapambana dhidi ya Eswatini na Madagascar, ikiwa ni maandalizi pia ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN), itakayoanza Agosti 2 hadi Agosti 30, 2025.

Wachezaji walioitwa ni Yakoub Suleiman, Abdulrahim Bausi na Wilson Nangu wa JKT Tanzania, Ally Salim, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Abdulrazack Hamza, Yusuph Kagoma, Valentino Mashaka na Kibu Denis wanaoichezea Simba.

Wengine ni Hussein Masalanga (Singida Black Stars), Antony Remmy (Azam U20), Mirajy Abdallah (Coastal Union), Mishamo Michael (KenGold), Ibrahim Ame, Idrisa Stambuli wanaoichezea Mashujaa na Selemani Mwalimu ‘Gomez’ (Wydad Casablanca).

Nyota wengine ni Lusajo Mwaikenda, Pascal Msindo, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Idd Seleman ‘Nado’ (wote Azam), Ibrahim Hamad ‘Bacca’, Dickson Job, Sheikhan Khamis (wote Yanga), Ahmed Pipino (KMC), Vedastus Masinde (TMA) na Simon Msuva (Al-Talaba).

Mwingine anayekamilisha kikosi hicho cha wachezaji 28, ni kiungo mkabaji, Alphonce Mabula Msanga anayechezea FC Shamakhi ya Azerbaijan.

Akitangaza kikosi hicho mapema leo Mei 31, 2025 katika Ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Kocha Morocco, amesema wanahitaji kutumia vyema mechi hizo kama njia ya maandalizi mazuri kwa ajili ya michuano mikubwa ijayo ya CHAN itakayoanza Agosti.

“Kuna baadhi ya wachezaji ambao wamekosekana hapo akiwemo nahodha, Mbwana Samatta ambaye niliwasiliana naye na akasema hayupo vizuri, pia kwa Clement Mzize na Mudathir Yahya wa Yanga wote ni majeruhi ila tutaungana nao baadaye,” amesema.

Morocco alisema kutokana na mechi ya Dabi ya Kariakoo kati ya Yanga na Simba iliyopangwa kupigwa Juni 15 mwaka huu, ametoa nafasi pia kwa wachezaji wa timu hizo kurudi Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi, hivyo haitawaathiri ndio maana wameita nyota wengi.

Kwa upande wa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Cliford Ndimbo, amesema nyota wote walioitwa wataingia kambini kuanzia Jumatatu ya Juni 2 huku Juni 3, kikosi hicho kitaanza safari ya kwenda Afrika Kusini.

The post 28 WAITWA TAIFA STARS….SAMATTA AOMBA POOO….MZINZE, MUDATHIR MHHH….. appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post WANAOTAKA KUTUSUA KIMATAIFA….HUU HAPA USHAURI WA MSUVA KWA MASTAA WA KIBONGO…
Next Post BAADA YA KUKOSA UBINGWA WA CAF….MANULA AVUNJA UKIMYA SIMBA…ATAJA MALENGO…
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook