Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Marekani Yamkamata Mtu kwa madai ya kujaribu kulipua ubalozi wake huko Israel

  • 40
Scroll Down To Discover

Raia wa nchi mbili za Marekani na Ujerumani alikamatwa Jumapili kwa madai ya kujaribu kulipua ubalozi wa Marekani huko Tel Aviv, Israel, kulingana na wizara ya sheria.

Maafisa walisema walimkamata Joseph Neumayer, 28, katika uwanja wa ndege wa John F Kennedy mjini New York.

Alikuwa amerejeshwa na mamlaka ya Israel baada ya kupatikana na vifaa vya vilipuzi kwenye mkoba karibu na ubalozi huo.

Bw Neumeyer alifikishwa mahakamani Jumapili na anazuiliwa gerezani, wizara hiyo ilisema.

“Mshtakiwa huyu anashtakiwa kwa kupanga shambulio baya lililolenga ubalozi wetu nchini Israel, likitishia vifo kwa Wamarekani, na maisha ya Rais Trump,” Mwanasheria Mkuu wa Serikali Pamela Bondi alisema.



Prev Post Musukuma Amchana Askofu Gwajima Bungeni Dodoma – Video
Next Post Majaliwa: Serikali itaendelea kuwaunganisha wafanyabiashara wa Kitanzania na mataifa mbalimbali
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook