

Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Kasheku ‘Musukuma’ amesema vyombo vya ulinzi na usalama vinapaswa kuwashughulikia wanaharakati wa Kenya wanaokuja nchini kufanya majaribio ya kuvuruga amani.
Akichangia hoja ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi bungeni jijini Dodoma, Mei 26, 2025 amesema wanasiasa nchini hawapaswi kuingilia maamuzi ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akimtaja Mbunge wa Kawe Askofu Joseph Gwajima kuingilia maamuzi ya Rais Samia kwa kutumia upole wake, kwani ni kuvuka mipaka na kuingilia mamlaka na kuliomba Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua wote wanaoingilia mamlaka.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!