MAGAZETI ya Leo Jumatatu 26 May 2025
Kocha wa Simba, Fadlu Davids anazungumzia mchezo akisema licha ya kupitia magumu mengi waliendelea kuwa imara na kupambana hadi mwisho wa mchezo, na kama timu wataendelea kuwa waadilifu.
Kocha Fadlu amegusia baadhi ya matukio ikiwemo kadi nyekundu kwa Yusuph Kagoma ambayo amesema “…haikuwa na ulazima….”
Kuhusu jinsi gani kadi hiyo imechangia matokeo ya leo, Fadlu amesema iliwaathiri kwakuwa walilazimika kucheza pungufu dhidi ya mabingwa wa Morocco, lakini haikuwapunguzia nguvu ya kusaka goli zaidi….
Kuhusu uamuzi wa ‘off-side’ kwenye kile walichoamini kuwa ni goli, Kocha Fadlu anasema hana uhakika kama kweli ilikuwa ni offside akisema “…sijaona mistari ya VAR kuonesha kuwa ilikuwa off side, na pia sijui kama kuna mtu ameiona, lakini tunakubali yote”
Amewapongeza wachezaji wake kwa upambanaji waliouonesha licha ya kuwa pungufu na kukabiliwa na maamuzi mengi yaliyokuwa dhidi yao…
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!