
MAGAZETI ya Leo Alhamisi 22 May 2025
MAGAZETI ya Leo Alhamisi 22 May 2025
Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Hashim Rungwe amesema ili Taifa lisonge mbele na Watu wapate nguvu ya kufanya kazi ni lazima wapate lishe bora akisisitiza kuwa msingi wa Taifa imara ni wananchi wenye afya bora hivyo sera ya Chama hicho ya kugawa ubwabwa Shuleni na Hospitali itaendelea.
Akiongea Jijini Dar es salaam May 21,2025 wakati wa mapokezi ya Wanachama wapya, Mzee Rungwe amesema kuwa Serikali ya CHAUMMA itahakikisha Watoto wanapata chakula, Watu wazima wanapata chakula, wanaoenda Hospitali wapate lishe, karibuni tujenge Taifa letu lililoshiba na wenye afya njema, walioshiba wataweza kupiga kura kwa utashi wao na hawatosubiri kupewa rushwa ya chakula ili wauze utu wao, twendeni tukajenge Taifa la ndoto zetu.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!