

Papa Leo XIV aliwahi kuitembelea Tanzania mwaka 2003 katika ziara yake ya kitume, ya kutembelea nchi za Afrika katika Provinsi mbalimbali za Shirika la Mtakatifu Augustino, wakati akihudumu kama Mkuu wa Shirika hilo kuanzia mwaka 2001 hadi mwaka 2013.
Wakati wa mahojiano maalum ya Mhashamu Stephano Lameck Musomba OSA, Askofu wa Jimbo Katoliki Bagamoyo aliiambia Radio Maria Tanzania, kuwa anamfahamu Baba Mtakatifu Papa Leo kwa sababu baada tu ya Upadre mwezi Julai 2003 wake alikuja Tanzania kwenye nyumba za Kitawa za Mapadre wa Augustiniani na aliendesha gari mwenyewe kutoka Jimbo Kuu Katoliki Songea hadi Jimbo Katoliki Morogoro.

Nchi Nyingine ambazo Baba Mtakatifu aliwahi kuzitembelea ni pamoja na nchi ya Ufilipino
kati ya mwaka 2002, 2010, na 2012, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) mwaka 2009, Kenya mwaka 2011, 2024, and 2025, Nigeria 2001 na 2016, Australia mwaka 2002 and 2005, Korea ya Kusini ambapo alishirikiana na Waagustiniani wenzake, kuanzisha nyumba ya Shirika mnamo mwaka 1985 na Nchini Peru ambapo Papa Leo alifanya utume wake kwa miaka zaidi ya 20.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!