Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Viongozi wa Ulaya Waungana na Zelensky Safari ya White House Kukutana na Trump

  • 32
Scroll Down To Discover

Baadhi ya viongozi wa Ulaya, wameamua kuandamana na Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine katika safari yake ya kwenda Washington katika hatua ya kidiplomasia ya kuunga mkono misimamo ya Ukraine katika mazungumzo yake na Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya mashinikizo ya nchi hiyo ya kumtaka akubali haraka makubaliano ya amani.

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, Keir Starmer Waziri Mkuu wa Uingereza, Friedrich Mertes, Kansela wa Ujerumani, Giorgia Meloni Waziri Mkuu wa Italia pamoja na Ursula von der Leyen, Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya ni miongoni mwa viongozi wa Ulaya watakaohudhuria mkutano huo na Trump. Kwa mujibu wa tangazo rasmi, Zelensky kwanza atazungumza na Trump akiwa peke yake na kisha viongozi hao wa nchi za Ulaya watashirikishwa katika hatua za baadaye za mazungumzo.

Zaidi ya miaka mitatu imepita tangu kuanza vita vya Ukraine, vita ambavyo vimekuwa na taathira kubwa katika ngazi za kimataifa. Kuongezeka kwa bei ya nishati, migogoro ya kiuchumi katika nchi tofauti na hasa changamoto za usalama katika mipaka ya Ulaya ni baadhi tu ya matokeo ya vita hivi.

Licha ya Rais Donald Trump wa Marekani kuahidi kumaliza vita na kuanzisha amani kati ya Ukraine na Russia, lakini hadi sasa hakuna dalili zozote za kumalizika vita hivyo. Kwa hiyo, katika wiki za hivi karibuni, hatua mpya zimechukuliwa ili kumaliza vita, ikiwa ni pamoja na mazungumzo ya karibuni kati ya Marais Trump wa Marekani na Vladimir Putin wa Russia huko Alaska.

Baada ya mazungumzo hayo, sasa Zelensky ameenda Ikulu ya White House kujadiliana na Rais wa Marekani kuhusu masharti na jinsi ya kuanzisha usitishaji vita na kupatikana amani nchini Ukraine.

Kutokana na sababu za kijiografia viongozi wa Ulaya wanavichukulia vita hivyo kuwa sehemu muhimu ya usalama wa nchi zao na ndio maana wamekuwa wakiunga mkono Ukraine tangu mwanzo wa vita na kuipatia kila aina ya silaha na vifaa katika miaka iliyopita, na wanaendelea kusisitiza msaada wao wa kiuchumi kwa nchi hiyo.

Lakini kwa nini wanaandamana na Zelensky sasa? Moja ya sababu muhimu ni kuzuia mashinikizo yanayoongezeka dhidi ya Kyiv, hasa kutoka kwa maafisa wa Marekani, kwa ajili ya kufikiwa makubaliano ya haraka ya amani. Rais Trump na wanasiasa wengine wa Marekani wanaamini kuwa kuendelea kwa vita kuna gharama kubwa kwa Marekani na dunia nzima kwa ujumla, na kwa hivyo vinapaswa kusimamishwa haraka iwezekanavyo. Mashinikizo yanaweza kusababisha kukubalika makubaliano ya amani ambayo ni hatari kwa Ukraine na maslahi ya muda mrefu ya Ulaya.

Nchi za Ulaya zina wasiwasi kwamba makubaliano ya aina hiyo ambayo hayana dhamana ya ushindi kwa Ukraine na kukombolewa maeneo yote yaliyotekwa na Russia, haswa katika hali ambayo nchi hiyo inaendelea kudumisha vitisho vyake, yataendeleza hali iliyopo hivi sasa na hata kuimarisha ushawishi wa Russia barani Ulaya.
Kwa upande mwingine, viongozi wa Ulaya wanaamini kwamba ikiwa Marekani itapunguza uungaji mkono wake kwa Ukraine, pengo hili litabakia kwa manufaa ya Russia,



Prev Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO AGOSTI 20, 2025
Next Post Mwili wa Mwanafunzi Aliyeuawa kwa Tuhuma za Wizi wa Simu Wapumzishwa Babati – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook