Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Tanzania Na Finland Zakubaliana Kuongeza Wigo Wa Ushirikiano

  • 26
Scroll Down To Discover

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Finland zimekubaliana kuanzisha maeneo mapya ya ushirikiano huku kipaumbele kikiwekwa zaidi kwenye masuala ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Hayo yameelezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Finland Mheshimiwa Alexander Stubb kwenye mkutano wao wa pamoja na waandishi wa habari uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam Mei 14, 2025.

Rais Samia ameyataja maeneo hayo ya ushirikiano kuwa ni uchumi wa buluu, madini, elimu, utalii, biashara na uwekezaji, misitu, uhifadhi wa mazingira, nishati, mafunzo ya kidigitali, ufundi stadi na nishati safi ya kupikia.

Rais wa Jamhuri ya Finland Alexander Stubb

Mbali na hayo Rais Samia ameizungumzia ziara hiyo kuwa imefungua zama mpya za ushirikiano katika Nchi hizo mbili rafiki, huku akiahidi kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Finland katika kutetea agenda mbalimbali za uwili na kimataifa ikiwemo ustawi wa uchumi wa watu, kulinda amani na usalama na utunzaji wa mazingira.

Kwa upande wake Rais wa Finland Mheshimiwa Stubb, ambaye ameambatana na ujumbe wa wafanyabiashara kutoka makampuni 10 ya nchini humo, ameeleza kuwa pamoja na masuala mengine ziara yake hapa nchini itasaidia kukuza ushirikiano wa sekta binafsi kupitia biashara na uwekezaji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Finland  Alexander Stubb wakati wakizungumza na Waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Mei, 2025.

“Finland inaitazama Tanzania kama mshirika wa kipekee katika bara la Afrika, daima tumekuwa na mitazamo inayofanana ya kutaka misingi ya sheria za kimataifa ziheshimiwe na kutekelezwa kwa usawa, kupigania usawa wa kijinsia, na amani na usalama. Hivyo ni imani yangu kuwa katika siku za usoni Finland na Tanzania tutakuwa wajumbe wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Mataifa”._ Alisema Mheshimiwa Rais Alexander Stubb.

Pamoja na masuala mengine Rais Stubb anatarajiwa kushiriki katika sherehe ya maadhimisho ya miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Finland itakayo fanyika kesho Mei 15, 2025 jijini Dar es Salaam.



Prev Post Zifahamu Nchi 10 Alizowahi Kuzitembelea Baba Mtakatifu Leo Xiv Kabla Ya Kuwa Papa, Tanzania Ni Mojawapo
Next Post MAGAZETI ya Leo Ijumaa 16 May 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook