
MAGAZETI ya Leo Jumatano 14 May 2025
MAGAZETI ya Leo Jumatano 14 May 2025
Serikali imesema kuwa ili kuhakikisha wanafunzi wote wanaomaliza darasa la sita wanakwenda sekondari, na wanafunzi wa mahitaji maalumu wanapata elimu bora ni lazima wanafunzi wote wa kada ya ualimu wawe na ujuzi wa lugha ya alama.
hayo yamesemwa Jumanne Mei 13,2025 na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026
Akizungumzia taarifa hiyo Mkenda amesema, Serikali inatarajia kuongeza miundombinu ya kutosha kwa kushirikiana na Wizara ya Tamisemi lakini pia kuongeza idadi ya walimu ili kuongeza ufanisi katika suala hilo lakini pia kuongeza ushirikiano na sekta binafsi.
“Kwenye sera yetu ya elimu, lugha ya alama itakuwa ni lazima kwa wanafunzi wote wanaosomea ualimu kwa sababu kama unafundisha shuleni lazima uweze kuwasiliana na wanafunzi wa aina wote bila vikwazo,” amesema Profesa Mkenda.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!