Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Vita Dhidi ya Kipindupindu Hanang’: Zaidi ya Wanafunzi 700 Wafaidika na Vyoo Vipya

  • 3
Scroll Down To Discover


Manyara 24 Agosti 2025: Kaya zenye vyoo bora nchini zimefikia asilimia 78 huku asilimia 1.2 hazina vyoo na kwa mkoa wa Manyara, asilimia 6.4 ya kaya hazina vyoo.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi anayeshughulikia Afya, Profesa Tumaini Nagu, kupitia hotuba iliyosomwa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Ibrahim Mbogo, amesema hali hii inahitaji ushirikiano wa serikali na wadau ili kuhakikisha kila kaya inakuwa na choo bora.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi wa kuboresha huduma za maji na usafi katika shule ya msingi Bashang, Prof Nagu amesema karibu asilimia 36 ya kaya za Hanang’ bado zinatumia vyoo visivyokidhi ubora, jambo linaloongeza hatari ya magonjwa ya mlipuko.

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la WaterAid Tanzania, Anna Mzinga, amesema mradi huo ni sehemu ya jitihada za kuhakikisha kila mtoto anajifunza katika mazingira salama na yenye huduma bora za maji na usafi wa mazingira, hatua itakayopunguza maradhi ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.

Katika shule ya msingi Bashang, zaidi ya wanafunzi 700 wamenufaika baada ya kujengewa vyoo vya kisasa vyenye matundu 23, miundombinu ya kuvuna maji ya mvua pamoja na vituo vya kunawa mikono. Wakitoa shukrani zao walimu wa shule hiyo wamesema mradi huo umeleta matumaini mapya ya mazingira bora ya kujifunza.

Mwanafunzi wa darasa la tano, Mathias Ombay akizungumza kwa niaba ya wenzake, amesema miundombinu hiyo imewapa faraja kubwa kwani awali walikuwa wakitumia vyoo visivyo salama hivyo ameahidi kuvitunza kwa kushirikiana na wenzake.

Mkazi wa Kijiji cha Bashang, Magdalena Lowri, ameishukuru serikali na wadau hao kwa kuwapelekea mradi huo, akisema utawasaidia watoto wao kusoma katika mazingira yenye usafi na salama kiafya.



Prev Post TRAMPA Yafika Gereza la Ukonga Kuonesha Matendo ya Huruma kwa Wafungwa
Next Post Wasira Amjulia hali Naibu Katibu Mkuu Mstaafu CCM Zanzibar Dr. Sadala
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook