Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Serikali Yazungumza na Marekani Kuhusu Dhamana ya Viza kwa Watanzania

  • 9
Scroll Down To Discover

Dar es Salaam, Oktoba 10, 2025 — Kuanzia Oktoba 23, 2025, Watanzania wanaoomba viza za utalii au biashara kwenda Marekani watahitajika kuweka dhamana ya kifedha (visa bond) itakayokuwa kati ya dola 5,000, 10,000 au 15,000 za Kimarekani, kulingana na uamuzi wa ubalozi wa Marekani.

Kiasi hicho cha dhamana hakihusiani na ada ya kawaida ya maombi ya viza, bali ni hatua ya ziada inayolenga kudhibiti tabia ya baadhi ya waombaji wanaobaki Marekani kinyume cha sheria baada ya muda wa viza zao kumalizika.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ubalozi wa Marekani, fedha hiyo itarudishwa endapo mwombaji atarejea Tanzania ndani ya muda halali wa viza yake. Hata hivyo, ikitokea amevuka muda wa viza (overstay), dhamana hiyo haitarejeshwa.

Hatua hii ni sehemu ya sera mpya za udhibiti wa uhamiaji zinazotekelezwa na Serikali ya Marekani kwa nchi ambazo raia wake wamekuwa wakionekana kukiuka masharti ya viza mara kwa mara.

Serikali ya Tanzania imesema inaendelea kujadiliana na Marekani kuhusu masharti hayo mapya, ikilenga kuhakikisha kwamba Watanzania wanaosafiri kwa nia halali hawataathirika na uamuzi huo.




Prev Post CCM Yawajibu ACT Wazalendo Kuhusu Hali ya Zanzibar
Next Post Dkt. Samia Akumbuka Urithi wa Baba wa Taifa Katika Ziara ya Butiama
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook