

Dar es Salaam 12 Mei 2025: Kampuni ya mtandao wa simu ya Vodacom Tanzania leo imeshiriki katika tukio la uzinduzi wa wiki ya ubunifu lililofanyika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo Mkurugenzi wa Fedha wa Vodacom Tanzania, Hilda Bujiku amewapongeza vijana wengi waliojitokeza kwenye wiki hiyo ya ubunifu na kuwataka kuendeleza bunifu hizo kwa manufaa ya taifa.

Mkurugenzi huyo pia amevisifu vyombo vya habari kwa mchango wake mkubwa wa kuandika habari za wabunifu mbalimbali jambo ambalo limekuwa likiwatia moyo katika kuendeleza vipaji vyao.
Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini Tanzania, John Rutere amesema anayo furaha kubwa ya kufanikisha uzinduzi huo ambao waliundaa kupitia progamu yao ya Funguo kwa kushirikiana na Vodacom, Costech na Mwananchi.

Huu ni mpango uliokusanya vijana wanaofanya shughuli za ubunifu kwasababu Tanzania inaendelea mbele na tunataka iende mbele zaidi hivyo basi Funguo program inasaidia vijana kwasababu wako na nguvu za kufanya uzalishaji na kutumia teknolojia mpya hivyo kuweza kusaidia taifa.

Katika mpango tumekuwa tukishirikiana na nchi rafiki kama vile Serikali ya Finland, Uingereza, UNDP Union, ambazo zimekuwa zikitusaidia pesa za kuwaendeleza hawa vijana na bunifu zao ambazo wanazianzisha.

Naye Pendo Mrema aliyefika kwenye uzinduzi huo kama kijana mbunifu alivipongeza vyombo vya habari kwa kuwasapoti wabunifu wa hapa nchini na kuwashauri vijana kujikita kwenye masuala ya kiubunifu wa kiteknolojia na kuachana na mizaa ya mitandaoni.
HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!