
MAGAZETI ya Leo Jumanne 13 May 2025
MAGAZETI ya Leo Jumanne 13 May 2025
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linapenda kuwafahamisha wadau wa mpira wa miguu na umma kwa ujumla kuwa kuanzia msimu ujao wa 2025/2026 litakuwa na mshirika (partner) wa michezo ya kubashiri katika mashindano yake yote.
Mshirika huyo atashikilia haki hizo kwa kipindi chote cha makubaliano.
Hivyo, yeyote mwenye nia au kuhitaji odds kwaajili ya mechi ambazo zitakuwa chini ya TFF atalazimika kuwasiliana na mshirika huyo.
Makubaliano ya TFF na mshirika huyo yatakuwa ni kwaajili ya odds tu, na si ushirika mwingine na kampuni za michezo ya kubashiri (betting companies) kama udhamini (sponsorship) au ushirikiano (partnership).
Utaratibu huu ndiyo unaotumika katika Ligi mbalimbali barani Ulaya.
Hatua hii ya TFF pamoja na mambo mengine, pia itazinufaisha kimapato klabu ambazo mechi zao zitakuwa zimeingia kwenye odds.
Licha ya malipo yatakayokuwa yanatokana na odds, bado klabu zitaendelea kudhaminiwa na kampuni hizo za michezo ya kubashiri, kwani utaratibu huu hauathiri makubaliano ya udhamini kati ya pande hizo.
Utaratibu wa kumpata mshirika huyo utafanyika kwa njia ya mnada utakaotangazwa wakati utakapowadia.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!